
                Kazi ya umisionari katika Unyamwezi ilianzishwa rasmi mwaka 1898 huko Urambo na wamisionari Edmund Dahls, Konrad Meiers na baadaye Rudolf Sterns kutoka Surinam kama mmisionari na kiongozi (Superintendent).
Misioni hii kwanza ilianzishwa na The London Missionary Society (LMS) mnamo mwaka 1878. Hata hivyo, kazi yao ya uinjilisti haikuwa na mafanikio makubwa kutokana na vurugu za kisiasa, ukosefu wa maelewano ndani ya wamisionari, tofauti za kijamii na kitamaduni, na utawala wa Kijerumani kuanzia 1890/91.
Kutokana na changamoto hizo, LMS walilazimika kuhamisha shughuli zao za umisionari kwa Kanisa la Moravian mwaka 1896/1897. Mazungumzo rasmi yalianza mnamo Aprili 1894 huko Ujerumani kati ya Board ya Misheni Herrnhut na LMS.
Ibada ya kwanza ya Kimoravian ilihudhuriwa na watu 500-600. Mahudhurio yalipungua, na wamisionari walibaini changamoto ikiwa ni pamoja na utegemezi wa zawadi, ushirikishaji wa uchawi, na vijana kuondoka kwenda kufanya kazi ya upagazi.
Wamoravian walianza misheni mpya katika Kitunda (1901), Sikonge (1902), Ipole (1903), Kipambawe (1904), na Usoke (1905). Safari ilikuwa ngumu sana: kutoka Urambo mpaka Kipambawe ilikuwa ni siku 17 kwa miguu.
Ubatizo wa kwanza ulifanyika 12 Aprili 1903 katika Misheni ya Kitunda ambapo Yohanes Kipamila na mkewe Maria Kipamila walibatizwa na kuwa Wamoravian wa kwanza Unyamwezini.
Tabora, Tanzania
info@mcwt.or.tz
(+255) 755 134 397
KUANZA KWA KANISA LA MORAVIAN TANZANIA MAGHARIBI - TABORA (UNYAMWEZI) Kazi ya wamisionari katika Unyamwezi ilianza rasmi mwaka 1898 huko Urambo, ikiwa na wamisionari Edmund Dahls, Konrad Meiers, na baadaye Rud...